Tuesday, November 10, 2009

MBULUMUNDU WAWA TISHIO MIKUMI

Jitihada za upandaji miti katika kijiji cha Mikumi zinazofanywa na asasi isiyo ya kiserikali ijulikananayo kama Greenbelt Schools Trust fund (GSTF) zimevamiwa na mbulumundu. Uvamizi huo mebainishwa wakati wa hughuli za usimamiaji na tathimini ambazo zimefanyika toka tarehe 4 hadi 6, Novemba, 2009 zilizofanywa na GSTF.

GSTF kupitia ufadhili wa shirika la kimataifa WWF kwa kusaidiana na wadau wengine imebaini kuwepo kwa changamoto kubwa inayopelekea kurudisha nyuma jitihada zinazofanywa na wanaharakati wa mazingira za uoteshaji wa miche ya miti ya aina mbalimabali ikiwemo jamii ya matunda kama vile michungwa malimao, miembe na mikwaju. Hatua hii imefuatia kutokana na kijiji hiyo kukumbwa na ukame na kupelekea shughuli za kiuzalishaji kushuka kwa kiwango kikubwa. Kwani asilimia 90% ya wakazi wa Mikumi hutegemea uzalishaji unaotokana na kilimo ilikujipatia kipato.

Katika kukabiliana na changamoto ya ukame, GSTF imeanzisha mradi wa upandaji miti kupitia kaya kwa kusaidiana na kamati za mazingira katika kijiji hicho. Hivyo katika hatua ya awali katika utekelezaji mradi, wanakamati walipewa mbegu ili wazioteshe.

Uvamizi wa mbulumundu umekuwa ukienda sambamba na jitihada za uoteshaji wa miche na kurudisha nyuma ukuaji wa miche hiyo.

Panzi hao wekundu wajulikanao kwa jina la Mbulumundu wamekuwa wakishambulia majani ya miche hasa majani laini yanayopatikana katika hatua za awali za uotaji wa miti. Bi Selina (mwanakamati) ameeleza akisema “Panzi hawa huwa wanahama wakiwa katika mamia au maelfu toka sehemu isio na mimea na kwenda sehemu inapoota mimea ilikujipatia chakula”. Ameendelea kueleza “… hii ni kutokana na ukame uliokithili uliosababishwa na kukauka kwa uoto wa asili hivyo mbulumundu wameamua kuvamia vitalu hivi’

Richa ya mbulumundu kushambulia vitaru vya miti, jitihada za uoteshaji miti zimezaa matunda. Kwani hivi sasa miche zaidi ya elfu moja (1000) imeoteshwa katika viriba, tayari kawa kuwasambazia wananchi ili waipande katika mvua za mwanzo.

GSTF kwa kushirikiana na wanakamati wa mazingira wamejipanga kupambana na mbulumundu kwa kuwatika mbegu nyingi za miti mara mvua za awali zitakaponyesha. Kwakuwa utafiti wa awali umeonesha kuwa panzi hao hufa kwa wingi kipindi cha mvua. Pia kuchipua kwa uoto wa asili kutapelekea panzi hao kwenda maeneo hayo na kutoa fulsa kwa mbegu za miti kuota vizuri katika vitalu na viriba.

Jitihada hizi zinafaa kuigwa na wadau mbalimbali , hasa katika masuala ya mazingira ilikukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayojitokeza hivisasa. Hasa katika katika kuwashirikisha wanajamii kupanda miti iliwamiliki misitu binafsi kwa matumi mbalimbali

Angelus Runji
runjifredy@yahoo.com

No comments:

Post a Comment